TUSKER YASHINDA POSTA RANGERS 2-1
Tusker FC imefufua matumaini yake katika Ligi Kuu ya SportPesa baada ya kuilaza Posta Rangers mabao mawili kwa moja uwanjani Ruaraka, Chris Erambo na Victor Mbaoma wakiifungia timu hiyo ushindi muhimu.
Matokeo hayo yameipandisha Tusker hadi nafasi ya kumi kwa pointi tisa, huku Kakamega Homeboyz ikiichapa Shabana mabao matatu kwa mawili baada ya kurejea mchezoni katika uwanja wa Bukhungu.
Nairobi United nayo ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu kwa kuilaza 3K FC mabao mawili kwa sifuri mjini Embu, huku Ulinzi Stars na AFC Leopards zikitoshana nguvu kwa sare tasa katika uwanja wa Nyayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

