Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

HIGHWAY YATWAA UBINGWA WA NAIROBI,

Shule ya Sekondari ya Highway imetwaa ubingwa wa soka wa shule za upili wa Mkoa wa Nairobi baada ya kuishinda Upper Hill kwa mikwaju ya penalti 4-3, kufuatia sare tasa katika mchezo wa fainali.

Ushindi huo umeipa Highway ubingwa wa mkoa kwa mara ya tatu mfululizo na kuihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mjini Thika baadaye mwezi huu.

Matokeo hayo yanaendeleza ubora wa Highway, mabingwa wa kitaifa wa mwaka 2024, ambao walionyesha utulivu mkubwa katika mikwaju ya penalti na kufanikisha ushindi huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *