Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

KAWAYA ASUTA UPINZANI KUHUSU UCHAGUZI WA 2027

Mbunge wa Mwala, Vincent Kawaya, amewashutumu viongozi wa upinzani kwa madai ya kuandaa mazingira ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 na huenda kuchochea machafuko nchini.

Kawaya amedai kuwa baadhi ya viongozi wanaotarajia kushindwa wanawaandaa wafuasi wao mapema kulaumu mchakato wa uchaguzi na hivyo kuhatarisha amani ya taifa.

Aidha, amekosoa viongozi hao kwa kujiondoa katika mkutano na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, akidai walikuwa wamepewa nafasi ya kuwasilisha malalamishi na mapendekezo yao badala ya kutafuta mzozo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *