Tuesday, November 24, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RUKU AONYA DHIDI YA SIASA ZA UKABILA NAIROBI

Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku amekosoa viongozi wanaotumia ukabila kutafuta uungwaji mkono wa kisiasa, akisema Nairobi inahitaji viongozi wenye uwezo wa kutatua changamoto za utoaji huduma.

Ruku amesema wanasiasa wanaohamasisha jamii kwa misingi ya kikabila hawana ajenda wala utaalamu wa kuleta mabadiliko katika mji mkuu.

Ruku, ambaye ametangaza nia ya kuwania ugavana wa Nairobi katika uchaguzi wa 2027, amesema wakazi wanahitaji uongozi utakaoboresha huduma muhimu na kuifanya Nairobi kushindana na miji mikubwa duniani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *