FAMILIA NYERI YALILIA KIFO CHA MTOTO SHULENI
Familia moja mjini Narumoru, Kaunti ya Nyeri, inaomboleza kifo cha mtoto wao wa miaka miwili na miezi tisa, Carlos Brown, aliyefariki akiwa shuleni.
Uongozi wa Shule ya Shalom umesema mtoto huyo aligongwa na basi la shule lilipokuwa likirudi nyuma.
Hata hivyo, familia ya marehemu imepinga maelezo hayo, ikidai yanakinzana na taarifa ya polisi, na sasa inataka uchunguzi wa kina pamoja na uwajibikaji kutoka kwa uongozi wa shule.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

