IEBC YAONYA WAPIGA KURA DHIDI YA KUKIUKA KANUNI ZA UCHAGUZI OLKALAU
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewaonya wapiga kura wa Ol Kalou dhidi ya kupiga picha au kusambaza picha za karatasi za kura zilizokwisha kupigwa alama wakati wa uchaguzi mdogo wa eneo hilo.
Tume hiyo imesema kitendo cha kupiga picha ya kura au kuisambaza ni ukiukaji wa sheria za uchaguzi na kinaweza kuhatarisha usiri wa kura pamoja na uadilifu wa mchakato wa uchaguzi.
IEBC imewataka wapiga kura kuzingatia taratibu za uchaguzi, kulinda siri ya kura zao na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha hatua za kisheria. Aidha, tume hiyo imewahimiza wananchi kujitokeza kwa amani na kushiriki katika uchaguzi kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

