Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

HENRY OMOLO AHAMIA LIGI YA ZAMBIA AKITOKEA KAKAMEGA HOMEBOYZ

Mshambuliaji wa Kakamega Homeboyz, Henry Omolo, amekamilisha uhamisho wa kudumu kwenda klabu ya Mufulira Wanderers nchini Zambia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye ana uwezo wa kucheza katika nafasi mbalimbali za ushambuliaji, anaondoka baada ya kuwa na msimu mzuri akiwa na Kakamega Homeboyz.

Omolo alichangia mafanikio ya timu yake kwa kufunga mabao matano na kutoa pasi tatu za mabao, huku Kakamega Homeboyz ikimaliza msimu katika nafasi ya tano.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *