RYAN OGAM AJIUNGA NA RFC LIÈGE KWA MKOPO
Mshambulizi wa Harambee Stars, Ryan Ogam, amejiunga na klabu ya RFC Liège ya Ubelgiji kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Wolfsberger AC ya Austria.
RFC Liège, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Ubelgiji, inatarajia mabao ya Ogam yataisaidia kupanda hadi Ligi Kuu katika msimu wa 2026/27.
Kwa Ogam, uhamisho huo unampa fursa mpya ya kufufua kiwango chake baada ya msimu wa kwanza uliokuwa na changamoto nchini Austria kufuatia kuondoka kwake kutoka Tusker FC mwaka uliopita.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

