ODEMBA ATAKA UWEKEZAJI ZAIDI KWA SOKA LA WANAWAKE
Kocha wa Harambee Starlets, Beldine Odemba, amesema kufuzu kwa Junior Starlets kwa Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 17 kunapaswa kuwa mwanzo wa uwekezaji wa kudumu katika soka la wanawake nchini.
Odemba ameitaka serikali pamoja na Shirikisho la Soka nchini (FKF) kuhakikisha timu hiyo inapata maandalizi na msaada wa kutosha kuelekea mashindano yatakayofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, 2026.
Aidha, amesisitiza haja ya kuboresha ustawi wa timu za taifa za wanawake, huku kukiwa na malalamiko yanayoendelea kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya posho za wachezaji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

