REAL MADRID YAIKOMESHA PSV KWA MABAO MATANO
Real Madrid imeendeleza rekodi yake nzuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuicharaza PSV Eindhoven mabao 5-1 Jumanne, huku Jude Bellingham akifunga bao la kuvutia katika ushindi huo uliowafanya mabingwa hao mara 15 kufikisha pointi 15 kutokana na mechi tano.
Hata hivyo, Arsenal na Manchester City zililazimishwa sare nyumbani, Arsenal ikitoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Borussia Dortmund, huku Manchester City ikilazimika kurejea kutoka nyuma mara mbili na kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Napoli.
Katika mechi nyingine, Como na Real Betis ziliendeleza mwenendo wao mzuri tangu kuanza kwa hatua ya ligi, huku Aston Villa ikipata kichapo kingine ugenini, na kuendeleza matokeo yasiyoridhisha katika kampeni hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

