Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

WAITITU KUSUBIRI HUKUMU NOVEMBA 2

Mahakama imepanga kutoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na washtakiwa wenzake Novemba 2, 2026, kufuatia kesi ya ufisadi na utakatishaji fedha inayohusisha shilingi milioni 588.

Wakati wa kusikilizwa kwa hoja za kupunguziwa adhabu, Waititu aliomba msamaha kwa mahakama kutokana na matendo yake, akiomba apewe adhabu nafuu na kueleza kuwa yeye pamoja na mkewe ni wahalifu wa mara ya kwanza.

Hakimu amesema hukumu rasmi itatolewa saa tano na nusu asubuhi Novemba 2, huku washtakiwa wengine wanaohusishwa na kesi hiyo wakiendelea kuzuiliwa akisubiri uamuzi wa mwisho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *