SOFAPAKA YAANZA KAMPENI YA NSL KWA USHINDI
Kocha wa Sofapaka Samuel Twago ana matumaini ya kuirejesha timu hiyo katika Ligi Kuu ya SportPesa baada ya kuanza kampeni ya Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza kwa ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Gucha Stars.
Nahodha Chris Situma alifunga bao pekee kwa mkwaju wa penalti katika mchezo uliofanyika Tendere Grounds, kaunti ya Kisii, huku Twago akisema ushindi huo ni hatua muhimu kuelekea kutimiza lengo la kupandishwa daraja lililowekwa na rais wa klabu Elly Kalekwa.
Twago pia amelitaka Shirikisho la Soka nchini FKF kutafuta mdhamini wa ligi hiyo, akisema ukosefu wa ufadhili unaathiri klabu nyingi, hasa zile za kijamii, huku akitumai msimu huu utaendelea bila usumbufu baada ya kuchelewa kuanza.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

