Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MBAPPE KUKOSA MECHI YA UFARANSA DHIDI YA ITALIA

Nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappe atakosa mechi ya Ligi ya Mataifa dhidi ya Italia mjini Milan kutokana na maumivu ya msuli wa nyuma ya paja, kwa mujibu wa kocha Zinedine Zidane.

Zidane amesema hataki kuhatarisha afya ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid, akitumai atarejea katika mechi dhidi ya Uturuki itakayochezwa Jumapili mjini Bordeaux.

Ufaransa inaongoza kundi A1 ikiwa na ushindi mara tatu na sare moja katika mechi nne, na ushindi dhidi ya Italia utaihakikishia nafasi ya kufuzu kwa robo fainali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *