ONYO LATOLEWA KUHUSU ATHARI ZA EL NIÑO NCHINI
Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu (IRC) limeonya kuwa hali ya hewa ya El Niño inazidi kuimarika na huenda ikasababisha mafuriko makubwa, milipuko ya magonjwa na ukame katika baadhi ya mataifa yaliyo hatarini.
Kenya, Uganda, Somalia, Bangladesh, Pakistan na Afghanistan zimetajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoweza kuathirika zaidi, huku baadhi yake tayari zikikabiliwa na changamoto za kibinadamu.
Kwa mujibu wa Kituo cha Marekani cha Utabiri wa Hali ya Hewa, kuna uwezekano wa asilimia 81 kwamba El Niño ya mwaka huu itakuwa miongoni mwa matukio makubwa zaidi tangu mwaka 1950, na inatarajiwa kufikia kilele kati ya Oktoba na Desemba.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

