Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

KAMPENI ZA OL KALOU ZAFUNGWA RASMI

Kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou zimefungwa rasmi kufuatia kuwadia kwa muda wa mwisho wa kufanya kampeni usiku wa jana.

Zaidi ya wapigakura 73,000 wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika Alhamisi kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge David Kiaraho mwezi Machi mwaka huu.

Hatua za mwisho za kampeni zilishuhudia misafara mikubwa ya magari, muziki na hotuba kali za kisiasa, huku upinzani ukidai matumizi ya rasilimali za serikali kushawishi wapigakura, madai ambayo yamekataliwa na viongozi wa Kenya Kwanza waliodai serikali inaendelea kutekeleza ajenda yake ya maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *