WAKAAZI WA MOREMBE WALALAMIKIA UKOSEFU WA UMEME
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Morembe, eneo la Magwagwa katika Kaunti ya Nyamira, wamelalamikia ukosefu wa huduma ya umeme kijijini humo, hali ambayo wanasema imeathiri shughuli zao za kila siku.
Wakazi hao wameitaka serikali pamoja na kampuni ya kusambaza umeme nchini, Kenya Power, kuingilia kati na kuhakikisha kijiji hicho kinaunganishwa na huduma ya umeme ili kuboresha maisha yao.
Wamesema upatikanaji wa umeme utachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku wakazi wakipata fursa ya kuanzisha biashara na kuboresha shughuli zao za kujikimu kimaisha.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo

