ETHEKON AMETAKA KANUNI ZA UCHAGUZI KUZINGATIWA
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC Erastus Ethekon, amevitaka vyama vya kisiasa kuzingatia kanuni za uchaguzi na kushirikiana na tume hiyo ili kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao yanafanyika kwa utaratibu.
Akizungumza katika kikao na viongozi wa vyama vya kisiasa jijini Nairobi, Ethekon amesema IEBC itachapisha sajili ya wapigakura mwezi Desemba mwaka huu ili kuwawezesha Wakenya kukagua na kuthibitisha taarifa zao.
Aidha, amesema tume hiyo itaendesha awamu nyingine ya usajili wa wapigakura katika miezi ya Januari na Februari mwaka ujao, ikiwa sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo

