MWADIME ATOA WITO WA KUMUUNGA MKONO RUTO
Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi na Ujuzi, Shadrach Mwadime, amewataka Wakenya kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kuchaguliwa tena, akitaja juhudi za serikali kuendeleza maeneo yote nchini.
Akizungumza mjini Voi, kaunti ya Taita Taveta, baada ya kuzindua vuguvugu la mashinani la Ruto Kumi, Mwadime amesema serikali ya Kenya Kwanza inatekeleza ahadi ilizotoa wakati wa kampeni.
Ametaja miradi ya maendeleo inayoendelea nchini, ikiwemo ujenzi wa viwanja vya michezo katika maeneo mbalimbali, akisema inalenga kukuza vipaji vya vijana na kuimarisha jamii.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

