IEBC YAPENDEKEZA KIWANGO KIPYA CHA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAMPENI
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imependekeza viwango vipya vya juu vya matumizi ya fedha za kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo, mgombea urais ataruhusiwa kutumia hadi shilingi bilioni 4.4, huku vyama vya kisiasa vikipewa kikomo cha matumizi ya takriban shilingi bilioni 17.7 wakati wa kampeni.
IEBC imesema mapendekezo hayo yanalenga kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi na kuhakikisha ushindani wa haki kwa wagombea na vyama vya kisiasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

