IEBC YAONYA DHIDI YA HONGO ZA UCHAGUZI
Kamishna wa IEBC, Dkt. Alutalala Mukhwana, ameonya kuwa kutoa au kupokea hongo wakati wa uchaguzi ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Uchaguzi.
Mukhwana amesema mgombea anayetoa fedha ili kuwashawishi wapigakura na mwananchi anayezipokea wote wanavunja sheria.
Aidha, amewahimiza wapigakura kufanya maamuzi kwa kuzingatia uwezo wa viongozi badala ya kushawishiwa na fedha au zawadi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

