Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

KENYA KWANZA YATETEA AJENDA YA SERIKALI

Viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza wameendelea kutetea utendaji wa serikali ya Rais William Ruto huku wakikosoa viongozi wa upinzani katika mikutano ya kisiasa iliyofanyika maeneo mbalimbali nchini.

Viongozi hao, akiwemo Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula, Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli, Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa na Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, wamewataka wananchi kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya serikali.

Wamesema serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na mipango ya kiuchumi ambayo tayari imeanza kuwanufaisha wananchi katika sehemu mbalimbali za nchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *