Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

WABUNGE WATATU WAMEJIUNGA NA DCP

Wabunge watatu wamejiunga na chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), kinachoongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, katika hatua inayodhihirisha kuimarika kwa chama hicho katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Hatua hiyo inajiri huku Gachagua akitangaza tarehe ya mwisho kwa viongozi wanaotaka kujiunga na DCP kutoka vyama vingine vya kisiasa, akiwataka kufanya hivyo kabla ya muda huo kukamilika.

Gachagua amesema hatua hiyo inalenga kuwezesha chama hicho kukamilisha maandalizi yake ya uchaguzi, ikiwemo kupanga mikakati na kuwatambua wagombeaji watakaokiwakilisha katika uchaguzi mkuu ujao.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *