ODM KUIMARISHA ULINZI WA NGOME ZAKE ZA KISIASA
Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimeimarisha msimamo wake wa kulinda maeneo kinayoyachukulia kuwa ngome zake za kisiasa, huku kikionya vyama vinavyoshiriki katika serikali jumuishi kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 utakuwa wa ushindani mkali.
ODM imesisitiza kuwa ushiriki wake katika serikali jumuishi hauimaanishi kuwa kimeachana na misingi yake ya kisiasa wala kujiondoa katika ushindani wa uchaguzi ujao.
Chama hicho kimeonya kuwa hakitakubali vyama vingine kupenya katika maeneo yake ya kisiasa bila upinzani, kikidokeza kuwa kiko tayari kupambana kuhifadhi uungwaji mkono wake katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo

