Thursday, July 30, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

POLISI WAONGEZA DORIA SABABU YA MAANDAMANO YA SABA SABA

Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS) imeimarisha vizuizi na doria za usalama katika barabara kuu za Nairobi wakati Wakenya wakiadhimisha Siku ya Saba Saba.

Polisi wamesema hatua hiyo inalenga kudumisha amani, usalama na utulivu wakati wa maadhimisho hayo ya kila mwaka.

Msemaji wa Polisi Michael Muchiri amesema uamuzi huo umetokana na matukio ya awali ambapo baadhi ya maandamano yaligeuka kuwa ya vurugu na kuvuruga shughuli za kawaida za wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *