EPRA: BEI YA MAFUTA ITABAKIA KAMA ILIVYO
Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA) imetangaza kuwa bei za juu za mafuta zitaendelea kubaki bila mabadiliko kwa siku 30 zijazo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jijini Nairobi, lita moja ya petroli itaendelea kuuzwa kwa Shilingi 214.03, dizeli kwa Shilingi 222.86, huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa Shilingi 191.38.
EPRA imesema hatua hiyo imewezekana kutokana na uingiliaji kati wa serikali unaolenga kuwalinda watumiaji dhidi ya mabadiliko ya bei katika soko la kimataifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

