Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MCA WA VIWANDANI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MADAI YA WIZI WA KIMABAVU

Mwakilishi wa Wadi ya Viwandani katika eneo Bunge la Makadara, Aaron Kang’ara Wangari, pamoja na washukiwa wengine wawili wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Makadara wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa Kimabavu.

Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), watatu hao wanadaiwa kuwashambulia watu watatu na kuwaibia fedha pamoja na mali nyingine katika eneo la Donholm mwezi uliopita.

Washukiwa hao wamekana mashtaka dhidi yao, huku mahakama ikiwapa dhamana ya Shilingi milioni moja kila mmoja au dhamana mbadala ya pesa taslimu ya Shilingi laki tano, wakisubiri kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *