UPINZANI WAKATAA MWALIKO WA IEBC, WATISHIA MAANDAMANO
Viongozi wa muungano wa upinzani wamekataa mwaliko wa IEBC wa kushiriki mkutano wa mashauriano kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027, wakitishia kuitisha maandamano makubwa iwapo matakwa yao hayatatekelezwa kufikia mwisho wa Desemba mwaka huu.
Viongozi hao wameishutumu tume hiyo kwa kushindwa kushughulikia kikamilifu malalamishi yao, wakitaka ukaguzi wa daftari la wapigakura pamoja na matokeo ya uchaguzi wa 2027 kutangazwa moja kwa moja kupitia matangazo ya moja kwa moja.
Miongoni mwa viongozi waliokataa mwaliko huo ni aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, Martha Karua wa PLP, Fred Matiang’i wa Jubilee na Ndindi Nyoro wa People’s Party of Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

