Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

WETANG’ULA AAGIZA UCHUNGUZI WA VIDEO YA SIMU ILIYOPOTEA BUNGENI

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula ameiagiza Kamati ya Mamlaka na Haki za Bunge kuchunguza video za kamera za usalama zinazohusishwa na madai ya kuibwa kwa simu ya mbunge ndani ya ukumbi wa Bunge mwaka 2023.

Agizo hilo limefuatia mabishano makali bungeni Jumatano, baada ya wabunge wakiongozwa na Sylvanus Osoro wa South Mugirango kutaka ufafanuzi kuhusu video ambayo Wetang’ula alisema ilionyesha mbunge mmoja akichukua simu ya mwenzake na kuiweka mfukoni.

Mbunge aliyeteuliwa Sabina Chege amesema simu hiyo iliyopotea ilikuwa yake na ilitoweka Juni 8, 2023, wakati wa kikao chenye vurugu ambapo alipata jeraha mkononi kabla ya kuondolewa ukumbini na maafisa wa Bunge na kupelekwa hospitalini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *