KWAMBOKA KUANZA SAFARI YA MARATHON VALENCIA
Bingwa wa Afrika wa mita elfu 10 Gladys Kwamboka anajiandaa kushiriki marathon yake ya kwanza mjini Valencia, Uhispania, Desemba 6, akilenga kuendeleza mafanikio yake katika mbio za barabarani.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 ataungana na Agnes Ng’etich ambaye pia atakuwa akianza marathon, pamoja na bingwa mtetezi Joyciline Jepkosgei na Lilian Kasait.
Kwamboka anaingia kwenye mashindano hayo akiwa na uzoefu wa mbio za nusu marathon, akiwahi kushinda Bogota mwaka 2024 na kumaliza wa tatu Yangzhou mwaka 2025.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

