Tuesday, November 24, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

CITY THUNDER KUKABILI MUNALI SUNS KASARANI

Mabingwa mara tatu wa Kenya, Nairobi City Thunder, wanatarajiwa kukutana na Munali Suns ya Zambia leo saa mbili usiku katika Uwanja wa Ndani wa Kasarani, katika mchezo wa pili wa mashindano ya kufuzu kwa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika, BAL, hatua ya Elite 16.

Thunder ilianza kampeni yake jana Jumatatu dhidi ya Urunani ya Burundi katika kundi A, huku mchezo wa leo ukiwa wa kwanza kukutanisha timu hizo mbili katika historia ya mashindano ya kimataifa.

Kikosi cha Kenya kimefuzu kwa mashindano makuu ya BAL katika misimu miwili iliyopita, 2025 na 2026, huku Munali Suns ikiingia hatua ya Elite 16 kwa mara ya kwanza, hali inayoweka ushindani mkali kati ya timu hizo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *