Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

OWINO AONGOZA GOR MAHIA KUTETEA TAJI

Nahodha wa Gor Mahia, Sylvester Owino, amesema kikosi hicho kimeazimia kutetea taji la Ligi Kuu ya SportPesa na kutwaa ubingwa kwa mara nyingine, akisisitiza kuwa timu hiyo lazima iendelee kupambana kwa bidii licha ya ushindani mkali unaotarajiwa.

Owino, aliyechukua unahodha kutoka kwa Philemon Otieno aliyestaafu mwezi Julai, alisaidia Gor Mahia kurejesha ubingwa msimu uliopita chini ya kocha Charles Akonnor, na sasa analenga kuiongoza timu hiyo kutwaa mataji mfululizo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25, aliyejiunga na Gor Mahia kutoka Kakamega Homeboyz mwaka 2022, amesema kutetea taji hakutakuwa rahisi na kikosi kinapaswa kudumisha kiwango bora ili kuwazidi wapinzani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *