IEBC YABORESHA HUDUMA ZA MTANDAONI
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza kutatizika kwa muda kwa baadhi ya huduma zake za mtandaoni kutokana na zoezi la kuboresha mifumo yake ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Hatua hiyo imefuatia malalamiko ya baadhi ya wapigakura walioshindwa kupata taarifa zao kupitia mfumo wa uthibitishaji wa usajili wa wapigakura.
IEBC imesema maboresho hayo ni ya kawaida na yanalenga kuimarisha huduma, huku ikiwahakikishia wananchi kuwa hitilafu hizo ni za muda na zitarekebishwa mara zoezi litakapokamilika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

