Thursday, November 26, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RUTO APINGA MASHARTI MAPYA YA UPINZANI

Rais William Ruto amekataa masharti mapya ya mageuzi ya uchaguzi yaliyotolewa na upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, akiyataja kuwa njama ya kuvuruga uchaguzi huo.

Akizungumza wakati wa kuanza ziara yake ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa Kenya, Ruto amedai kuwa viongozi wa upinzani tayari wanatambua kushindwa kwao katika uchaguzi ujao.

Kuhusu matakwa ya upinzani kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, rais amesisitiza umuhimu wa kulinda uhuru wa tume hiyo, huku akiishutumu kambi ya upinzani kwa kuweka msingi wa kuzuia uchaguzi baada ya kutarajia kushindwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *