OMONDI YUPO TAYARI KUZIMA MOTO WA BAFANA BAFANA
Kipa wa Harambee Stars Byrne Omondi anatarajiwa kuwa kikwazo tena kwa Afrika Kusini katika mechi ya kufuzu kwa AFCON 2027 itakayochezwa hii leo katika Uwanja wa Nyayo
Omondi aliokoa Kenya mara kadhaa katika sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Bafana Bafana mjini Johannesburg Ijumaa, akionesha umahiri licha ya mashambulizi ya mara kwa mara ya wenyeji
Kipa huyo wa Gor Mahia aliweza kuzuia shuti la Iqraam Rayners aliyekuwa amepenya na kuelekea langoni, na sasa analenga kuendeleza kiwango hicho katika mechi ya marudiano hio.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

