OBURU AMHIMIZA RAIS RUTO KUWA MKAKAMAVU KATIKA MAAMUZI YANAYOHUSU TAIFA
Kiongozi wa ODM Oburu Odinga amemtaka Rais William Ruto kuonyesha uongozi thabiti na usioyumbishwa wakati wa kufanya maamuzi magumu yanayohusu maslahi ya taifa.
Seneta huyo wa Siaya amesema uongozi wenye maamuzi ya ujasiri unahitajika ili kuhakikisha Kenya inalinda na kuimarisha mustakabali wake wa kiuchumi.
Oburu amesema alimpa Rais Ruto ushauri wa wazi kuhusu uongozi, akimtaka kubaki imara katika kutekeleza sera zinazolenga maslahi ya muda mrefu ya nchi licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

