FIKIRINI JACOBS AHOJIWA KUHUSU KIFO CHA CECIL OUMA
Katibu Mkuu wa Masuala ya Vijana, Fikirini Jacobs, ametoa taarifa kwa polisi kufuatia madai yanayohusishwa na mauaji ya mhamasishaji wa kisiasa Cecil Ouma, aliyepatikana ameuawa ndani ya gari linalodaiwa kuhusishwa naye.
Fikirini, aliyejitokeza katika Makao Makuu ya Polisi ya Kaunti ya Nairobi, amesema anashirikiana kikamilifu na maafisa wa uchunguzi ili kuhakikisha ukweli unabainika na haki inatendeka.
Uchunguzi wa maiti umebaini kuwa Ouma alifariki kutokana na jeraha la risasi moja lililopenya kwenye pafu, huku risasi hiyo ikipatikana kwenye uti wa mgongo huku Maafisa wa IPOA wakichukua risasi hiyo kwa uchunguzi wa kitaalamu wa balistiki kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

