Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

WATU KUMI WAKAMATWA MAANDAMANO YA SABA SABA

Polisi waliwakamata watu kumi katika eneo la Biashara la Nairobi kwa kushiriki maandamano ya Saba Saba yaliyofanyika hapo jana.

Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amesema maandamano hayo yalikuwa kinyume cha sheria kwa kuwa polisi hawakupokea notisi inayotakiwa kisheria kabla ya kufanyika kwake.

Hata hivyo, makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa hatua hiyo, yakidai kuwa imekiuka haki ya kikatiba ya wananchi ya kukusanyika kwa amani, huku yakisema yalinuia kuwasilisha bungeni ombi la fidia kwa waathiriwa wa maandamano ya mwaka uliopita.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *