ZAIDI YA WANAFUNZI 57,000 WAKOSA NAFASI VYUO VIKUU
Zaidi ya wanafunzi 57,000 waliotimiza vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu hawajapata nafasi katika kozi za shahada, kulingana na matokeo ya hivi karibuni yaliyotolewa na KUCCPS.
Wizara ya Elimu imeongeza muda wa kurekebisha maombi ili kuwapa wanafunzi walioathirika nafasi ya kutuma upya maombi ya kozi zilizosalia.
Wakati huo huo, zaidi ya wanafunzi 200,000 wamepangiwa nafasi katika vyuo vikuu, vyuo vya kati na taasisi nyingine za elimu ya juu, huku kozi za tiba na elimu zikiongoza kwa idadi ya waombaji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

