Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MAREKANI YAFUZU HATUA YA 16 BORA BAADA YA KUICHAPA BOSNIA

Marekani imefuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Bosnia na Herzegovina mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Jumatano.

Folarin Balogun aliifungia Marekani bao la kwanza mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu, huku wenyeji wakidumisha ubabe wao hadi mwisho wa mchezo na kuandika ushindi wao wa pili pekee katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia.

Kwa ushindi huo, Marekani sasa itavaana na Belgium katika hatua ya 16 bora, huku mashabiki wakitarajia pambano kali kati ya mataifa hayo mawili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *