AKONNOR ATAKA UWANJA WA DANDORA USICHEZEWE MECHI ZA LIGI KUU
Kocha wa Gor Mahia, Charles Akonnor, ameonyesha kutoridhishwa na hali ya Uwanja wa Dandora, akisema haukidhi viwango vinavyohitajika kuandaa mechi za Ligi Kuu ya FKF.
Akonnor amesema Gor Mahia ilicheza mechi kadhaa katika uwanja huo msimu uliopita, lakini anaamini ubora wa uwanja huo umeathiri kiwango cha mchezo licha ya timu yake kutwaa ubingwa wa msimu wa 2025/26.
Aidha, amelitaka Shirikisho la Soka Kenya (FKF) kuondoa Dandora kwenye orodha ya viwanja vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu hadi litakapoboreshwa na kufikia viwango vinavyohitajika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

