SENETI YAIBUA WASIWASI KUHUSU UFADHILI WA MANISPAA ZA KAUNTI
Kamati ya Seneti kuhusu Ugatuzi imeeleza wasiwasi wake kuhusu kushindwa kwa baadhi ya serikali za kaunti kutenga fedha za kuendesha manispaa.
Maseneta hao, waliokutana na viongozi wa Kaunti ya Bungoma wakiongozwa na Gavana Kenneth Lusaka, wamehoji sababu ya kuanzishwa kwa manispaa ikiwa hazitengewi hata mapato yanayokusanywa ndani ya maeneo hayo.
Kamati hiyo imezitaka serikali za kaunti kuhakikisha manispaa zinapata rasilimali za kutosha ili ziweze kutekeleza majukumu yake na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

