Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

OWALO AZINDUA CHAMA KIPYA CHA KISIASA

Aliyekuwa Waziri wa Habari na Teknolojia, Eliud Owalo, amezindua chama kipya cha kisiasa kitakachojulikana kama People’s Prosperity Party, akisema atakitumia kuwania urais katika uchaguzi ujao.

Owalo amesema kipaumbele chake kikuu kitakuwa kuimarisha uchumi na kuboresha maisha ya wananchi iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Aidha, amezisuta serikali zilizopita kwa kushindwa kutatua changamoto zinazowakabili Wakenya na kuahidi kutoa mwelekeo mpya wa maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *