Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

SERIKALI YASEMA HUSTLER FUND HAITAFUTWA

Katibu Mkuu katika Wizara ya Ushirika, Mang’eni, ametetea mpango wa Hustler Fund, akisisitiza kuwa serikali haina mpango wa kuufuta licha ya mijadala kuhusu mustakabali wake.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge, Mang’eni amesema mfuko huo unaendelea kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara wa mashinani kupata mikopo, hasa wale ambao hawana fursa rahisi ya kupata huduma za mikopo kutoka benki.

Serikali imesema Hustler Fund ni sehemu muhimu ya mpango wake wa kuwawezesha wananchi kiuchumi na kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *