Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RAIS WILLIAM RUTO AMEKUTANA NA RAIS WA UJERUMANI

Rais William Ruto amekutana na Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, katika Ikulu ya Nairobi, ambapo viongozi hao wamejadili mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Ujerumani.

Mazungumzo hayo yamelenga kupanua fursa za biashara na uwekezaji, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali zenye manufaa kwa mataifa hayo mawili.

Viongozi hao wameelezea dhamira yao ya kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Kenya na Ujerumani, kwa lengo la kukuza maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *