UFARANSA NA UHISPANIA KUKUTANA NUSU FAINALI HII LEO
Mabingwa wa dunia mara mbili Ufaransa watamenyana na mabingwa wa Ulaya Uhispania katika nusu fainali ya Kombe la Dunia, huku kila timu ikisaka nafasi ya kutinga fainali.
Mchezo huo utachezwa jijini Dallas, na mshindi atakutana na mshindi wa pambano kati ya England na Argentina katika fainali.
Ufaransa inalenga kufuzu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mfululizo, huku Uhispania ikisaka tiketi ya pili pekee ya kucheza fainali tangu ilipotwaa ubingwa mwaka 2010. Timu zote mbili zimeonyesha kiwango bora katika mashindano ya mwaka huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

