Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MUSONYE: MAANDALIZI YA AFCON 2027 YAPO NJIANI LICHA YA CHANGAMOTO

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya AFCON 2027, Nicholas Musonye, amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri licha ya kuwepo kwa changamoto mbili kuu zinazokabili mchakato huo.

Musonye amesema uzoefu uliopatikana kupitia maandalizi na uandaaji wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) 2024 unatumika kuboresha maandalizi ya AFCON 2027.

Aidha, amesisitiza kuwa kamati inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Kenya inakuwa tayari kuandaa kwa mafanikio mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *