Monday, October 5, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

MOTO WATEKETEZA BIASHARA ENEO LA GATAKA RONGAI

Wafanyabiashara katika eneo la Gataka, Rongai wanahesabu hasara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuteketeza mali katika majengo yaliyo mkabala na Duka kuu la Destiny mwendo wa saa kumi asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, moto huo unashukiwa kusababishwa na mlipuko wa gesi, ingawa chanzo kamili bado hakijathibitishwa.

Maafisa wa zimamoto walifika eneo la tukio kujaribu kudhibiti moto huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha mkasa huo na kiwango cha hasara iliyosababishwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *