Wednesday, November 25, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

OBURU OGINGA AREJEA BUNGENI BAADA YA KUUGUA

Seneta wa Siaya na kiongozi wa ODM, Dkt Oburu Oginga, amerejea katika shughuli za Bunge la Seneti baada ya kukaa nje kwa wiki kadhaa kutokana na kuugua, akipokelewa kwa shangwe na maseneta wenzake.

Akizungumza baada ya kurejea, Oburu amewataka Wakenya kukataa siasa za migawanyiko na kukumbatia umoja, akisema tofauti za kisiasa hazipaswi kuzuia viongozi na wananchi kudumisha mahusiano mema.

Aidha, amewashukuru Wakenya kwa jumbe na maombi ya kumtakia nafuu wakati alipokuwa kitandani, akisema upendo na faraja yao vilimpa nguvu ya kukabiliana na hali hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *