WAZIRI OGAMBA AFIKA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA ELIMU
Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba amefika mbele ya Kamati ya Bunge ya Elimu kujibu maswali kuhusu hatma ya vyuo vya mafunzo ya kiufundi nchini.
Wajumbe wa kamati wanatarajiwa kuhoji wizara kuhusu changamoto zinazoathiri vyuo vya kiufundi na namna serikali inavyopanga kuhakikisha taasisi hizo zinapata ufadhili wa kutosha ili kuendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi.
Mjadala huo pia unalenga kupata ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kuboresha elimu ya kiufundi na kuhakikisha vyuo hivyo vinaendelea kutoa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira.
Imetayarishwa na Hilda Ajema

