Wednesday, July 29, 2026

Nairobi 97.7 Western 89.3 Eldoret 92.3 Kitui 105.6 Taita 94.9 North Rift 84.7 Kibwezi 87.9

RISASI ZATIBUA MKUTANO WA KANG’ATA NYAHURURU

Mkutano wa kisiasa wa Gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata ulitibuliwa na ghasia katika mji wa Nyahururu, Kaunti ya Nyandarua, baada ya watu wanaodaiwa kuwa wahuni kuvamia msafara wa Linda Mwananchi.

Katika vurugu hizo, dereva wa Kang’ata alipigwa risasi kifuani huku viongozi kadhaa wa muungano huo wakijeruhiwa.

Baada ya tukio hilo, viongozi wa Linda Mwananchi wameisuta serikali wakidai ilituma wahuni kuvuruga shughuli zao za kisiasa, madai ambayo hayajajibiwa rasmi na serikali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *